Monday, February 11, 2013

Harakati za kumuona Chui huko Serengeti Asubuhi hii

 Serengeti National Park
Ni Leo Asubuhi kwenye eneo maarufu lijulikanalo kama 16 (kumi na sita) ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti. Hizi zimerushwa na mdau Thomas wa HSK Safaris aliyeoko huko Serengeti hivi sasa. Taswira zaidi zitakuja baadae, endelea kuwa nasi.

Serengeti National Park
Eneo hili ni eneo maarufu kwa kuonekana Chui maarufu kama Wa Juu. Leo wadau waliopo huko porini walipata fununu za uwepo wake maeneo haya hivyo kila mmoja aliamka na kutimua mbio kufika hapa ili kumuwahi. Bila mafanikio wajuu huyo hakuweza kuonekana kirahisi. inapotokea hali kama hii, basi gari linaweza kuchukua mwelekeo mwingine lakini eneo kama hili linaweza kurudiwa mida mingine kama ratiba ya mgeni inaruhusu.
Shukran kwa mdau Thomas wa HSK safaris

No comments:

Post a Comment