Thursday, January 3, 2013

Stesheni ya Mzenga, Kisarawe

Ni Stesheni ya treni ya TAZARA iliyopo huko Mzenga Kisarawe. Stesheni hii ipo baada ya kupita Stesheni ya Mwakanga, Stesheni ambayo commutter train aka Treni ya Mwakyembe huishia/kuanzia.

Mara kadhaa mwenyekiti wa Jukwaa la Mjengwa Blog (Maggid Mjengwa) amekuwa akitueleza mambo mbalimbali kuhusu Mzenga ambako ni kwa wajomba zake. Kwa lugha nyingine Mama yake Mwenyekiti ni mzaliwa wa Mzenga (kama sikosei). Jicho la Tembea Tz lilipita hapa mwishoni mwa mwaka jana likiwa kwenye treni maalum ya kupeleka watalii kwenye pori la akiba la Selous.

"Lines man" wa stesheni ya Mzenga akiwa bize kuhakikisha usalama wa Treni maalum kati ya kituo cha mzenga na kituo kinachofuata.

3 comments:

  1. Nimefurahiswa na mpango huu wa kutembelea mbuga za wanyama,safari hii lazima niwemo.

    ReplyDelete
  2. Nimefurahia mpango huu,nitakuwepo katika safari ya kwenda kutembelea mbuga.

    ReplyDelete