Thursday, January 3, 2013

Eneo la chemchem ya Maji Moto, Kisaki

 Kimsingi hapa ndipo tulipogeuza na Treni na kurudi Dar. Ni eneo ambalo lipo kilometa chache baada ya kupita stesheni ya Kisaki. Kuna chemchem ya maji ya moto kama inavyoonekana picha juu na ndio ambako ile Bush party ilipofanyika (eneo pembeni na chemchem). Treni ilisimama na abiria wote tukaambiwa tushuke. Baada ya abiria kushuka Treni ilirudi stesheni ya Kisaki kufanya shunting na baadae kurudi hapa ilipotuacha ili kutuchukua.

Baada ya kufika wasafiri wengi walikuwa na shauku ya kuyakaribia na kuona joto la hayo maji moto. Kwani tulipokuwa tukitangaziwa, tuliambiwa kuwa joto la maji ya chemchem hii linaweza kuchemsha hata yai. Hakuna aliyepingana na kauli hii. Maji ni ya moto na yanaweza kukuunguza kama hutachukua tahadhari madhubuti. Kimsingi, huweza kuoga maji ya hii chemchem bila kuyachanganya na maji baridi, Utababuka. Watalii wakichukua sampuli za maji hayo baada ya kuambiwa yanasaidia kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo Fangasi. Hapa safari ya utalii iligeuka kama ya kwenda kwa babu vile. Ghafla chupa tupu za maji ziligeuka kuwa dili.

Ni maji ambayo yana Sulphur nyingine kama inavyoonekana 

Wadau wa Clouds TV wakimhoj mzee ambae amekuwa akiishi eneo hili tokea mwaka 1946.

Wakati wengine wakiwa bize kwenye maji moto, wengine walikuwa wanaendelea kula bata la Bush party


Treni ikiwa imeshageuza tayari kwa safari ya kurudi dar. Ilichukua abiria na kuwapeleka Stesheni ya Kisaki ambako tulisimama kwa muda kupata msosi wa mchana kabla ya kuanza safari ya kurudi Dar ilipotimu saa kumi kamili jioni. Hili eneo lipo nje ya pori la akiba la Selous.

No comments:

Post a Comment