Wednesday, January 23, 2013

Safari za ATCL kwenda Kigoma zarejea

Shirika la Ndege la Tanzania, ATCL, limerejesha safari za ndege yake aina ya Dash 8 baada ya matengenezo ya kioo chake kilichopata nyufa ikiwa njiani kurejea Dar kukamilika. Ndege hii ilipata tatizo hilo muda mfupi baada ya kuruka toka uwanja wa Kigoma ikiwa ni safari ya kwanza kwa ATCL mara baada ya uwanja wa ndege wa Kigoma kufunguliwa baada ya matengenezo. Safari za kwenda na kurudi Kigoma kwa ndege za ATCL zipo siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili. Pichani ni Abiria wakipanda ndege hiyo katika uwanja wa Kigoma baada ya kukamilika kwa matengenezo ya ndege inayotumika kwenye safari hizo. 
Picha ni kutoka ktk FB wall ya Air Tanzania

2 comments:

  1. lakini bado mbovu

    ReplyDelete
  2. Ingekuwa mbovu ingeruhusiwa kufanya safari? kuwa mstaarabu basi.


    ReplyDelete