Tuesday, January 29, 2013

Hatukuzisoma alama mapema..

Camping in Mikumi NP with lakeland Africa
Sharubu ambae tulimuona pembezoni ya bwawa la Viboko (karibu na Campsite) tungeweza kumuona mapema zaidi kama tungeweza kusoma viashiria vya ndege hawa ambao walikuwa pembezoni ya korongo. Kanga hawa walikuwa kwenye hali ya kuhamaki hali ya inayoashiria kuwa kuna kitu kisicho cha kawaida ambacho kilikuwa kwenye korongo mbele yao. Kwa kuwa hii ilitokea karibu kabisa na bwawa la Viboko, eneo ambalo wengi walikuwa na hamu ya kufika na kushuka, hakuna aliyeweza kusoma viashiria hivyo na kuangalia zaidi kilichomo korongoni.

Camping in Mikumi NP with lakeland Africa
Ukweli ni kwamba kwenye korongo ambapo juu yake tuliwakuta kanga hao juu kulikuwa na sharubu dume aliyekuwa amelala kwa utulivu. Awali tulimpita na kwenda mpaka hippo pool na kushuka na kisha kupiga picha. Baadae tukapanda lorry na kuendelea na safari ambapo mita chache tu baada ya kuondoka bwawa la viboko tulikutana na gari nyingine ambayo ilituambua kuwa huko tunapotoka kulikuwa na sharubu. ndipo tulipogeuza na kurudi pale tulipoelekezwa (pembeni ya bwawa la viboko) tulimkuta sharubu anayeonekana akiwa amelala kwenye nyasi. Alikuwa ni sharubu wa kwanza kuonekana baada ya kuanza evening game drive. Safari hii tulipata bahati ya kuona Sharubu dume tu.

Camping in Mikumi NP with lakeland Africa
Hapa akiwa anaoenkana kwa karibu. Alikuwa amedhoofu huku sehemu ya shingo ikiwa na majeraha. Kuonekana kwake eneo hili ambalo lipo karibu na campsite tuliyofikia kulichangia wadau kutolala mapema huku kila mara tochi zikiwa zinamulikwa kwenye maeneo yanayoizunguka camp ili kujaribu kumbaini kama atakuwa kasogea na tulipoweka kambi.

1 comment: