Monday, December 31, 2012

Walidhania ni Treni ya Mwakyembe..

 Muda mfupi baada ya Treni maalum ya kutembelea pori la akiba la Selous kuondoka katika stesheni ya TAZARA hapa Dar Es Salaam, mtoa matangazo alisikika akisema ya kuwa kuna abiria walipanda treni hiyo kimakosa wakidhani ni treni ya Mwakyembe (Commuter train) ambayo huishia stesheni ya Mwakanga. Hakuna abiria aliyeacha kuangua kicheko kwa tangazo hilo hali iliyofanya wengi kuwa na shauku kubwa ya kuwaona abiria hao waliojichanganya tulipofika stesheni ya Mwakanga ambapo ndipo waliposhushwa. Picha hizi mbili kuna vijana wawili ambao ndio hao waliopanda kwa kudhania ni Treni ya Mwakyembe na kuja kubaini siyo. Walishushwa stesheni ya Mwakanga kama wanavyoonekana ktk picha hizi mbili.

Siku za weekend na siku za sikukuu, commuter train aka Treni ya Mwakyembe hazitoi huduma.

No comments:

Post a Comment