Thursday, December 27, 2012

Delta ya Mto Wami

 Mdau Abdul Kimanga wa Respect Djs Alikuwa kwenye hifadhi ya taifa ya Saadani kipindi hiki cha sikukuu ambapo alipata fursa ya kutembelea eneo ambapo mto wami unaingia baharini. Ni eneo ambalo lipo mpakani mwa hifadhi ya Saadani na vijiji lakini kutokana na uwepo wa wanyama kama viboko na mamba, TANAPA wanalisimamia na kuratibu shughuli eneo hilo. Kuna safari za boat ambapo mgeni hulazimika kupata kibali toka TANAPA na kisha kukodi boti itakayotembeza na kumzungusha kama alivyofanya mdau Abdul.
Saadani ni moja ya hifadhi mbili zilizopo Africa ambapo Bahari hukutana/kupakana na Hifadhi ya taifa yenye wanyama wa porini. Nyingine ipo Afrika Magharibi.


Eneo hili lina viboko wa kutosha.


Picha zote na Mdau Abdul Kimanga wa Respect Djs

No comments:

Post a Comment