Thursday, December 27, 2012

Boxing day ndani ya Kisiwa cha Mbudya, Dar Es Salaam

Mbudya ni kisiwa kilichopo ukanda wa Kunduchi kwenye pwani ya jiji la Dar. Kinafikika kwa boti ambazo huanzia kwenye hoteli mbalimbali zilizopo ukanda wa pwani ya Kunduchi. Ni kisiwa ambacho kipo ndani ya eneo la hifadhi ya viumbe wa majini (marine reserve) linaloitwa Mbudya Marine Reserve. Kisiwa hiki kipo chini ya usimamizi wa wizara ya uvuvi, japo ni kivutio kwa utalii. Ni sehemu murua kwa mapumziko ya pwani hususan kwa wale wanaopenda kuogelea na wasioogopa usafiri wa boti. 26 Desemba 2012, Kamera ya Tembea Tanzania ilienda kisiwani huko kwa kupitia boti zinazoondokea Hoteli ya White sands. Kusema ukweli kulikuwa na watu wengi wa kada mbalimbali na wote walikuwa na lengo la kutafuta eneo mwanana la pwani ili waweze kupumzisha akili na miili yao. Picha juu ni pwani mojawapo iliyopo kisiwa cha mbudya kama inavyoonekana tokea kwenye boti wakati wa kwenda mbudya.

 Maji ya Bahari huwa na kupwa na kujaa, kwa anayependa kuogelea hali ya maji kupwa inamnyima starehe yake mwogeleaji. Kisiwa cha Mbudya, haijalishi kama ni maji kupwa au kujaa (huku nchi kavu) daima kunakuwa na kina cha maji ya kutosha kwa mtu mzima kuogelea na kamwe asijue kama ni maji kupwa au kujaa. Hii ni moja ya sifa inayowapeleka wengi kuogelea Mbudya kwani huna haja ya kufuatilia utabiri wa hali ya hewa kujua hali ya kina cha maji kwa siku unayotaka kwenda kuogelea. Picha juu ni wadau mbalimbali waliofika kwa namna tofauti tofauti wakifurahia mchanga mwanana wa pwani ya kisiwa cha Mbudya.

 Tupo ambao tulienda kuwa usafiri wa 'umma' boti za wengi na wengine walikuja kwa boti binafsi. Na sio boti tu, wapo waliofika hapo kwa njia ya JetSki. Ukiangalia picha hii utaona boti moja ikisindikizwa na jetski mbili kila upande wakiingia kisiwa cha Mbudya kwa mbwembwe na madaha.







Wengine waliingia kwa usafiri wao kama unavyoonekana ukiwa parking  mchangani Mbudya.

No comments:

Post a Comment