Thursday, November 8, 2012

Mdau Atembelea Hifadhi ya Kisiwa cha Saa nane Mwanza

Ni Mdau Abdul wa Respect Djs ambaye alitenga muda wake na kuamua kutembelea kisiwa cha saa nane kilichopo ktk jiji la Mwanza.

Tumbili wapo wa kutosha tu kisiwani hapo.

Ofisi za wasimamizi wa hifadhi ya Taifa ya Saa Nane. Awali kisiwa hiki kilikuwa ni hifadhi lakini mwanzoni mwa mwezi wa Tisa mwaka huu, Bunge limekipandisha hadhi na kukifanya kisiwa hiki kuwa Hifadhi ya Taifa na kuwa chini ya usimamizi wa TANAPA.

Kisiwa cha Saa nane kinafikika kwa njia ya boti tokea jiji la Mwanza. Boti inayoonekana juu ndio iliyompeleka Mdau Abdul mpaka Kisiwa cha Saa Nane tokea Mwanza mjini.

Mdau Akiwa kwenye boti tayari kwa kuanza safari kuelekea Kisiwani. Hapa ni akiwa upande wa Mwanza mjini

(Picha kwa hisani ya mdau Abdul wa Respect Djs)

No comments:

Post a Comment