Wednesday, October 17, 2012

Trekking Safari in the rift valley with Tanzania Travel Company

Trekking Safari  ni safari ambayo mgeni hutumia muda mwingi wa safari yake (au kipande cha safari) akitembea kwa miguu. Tofauti kati ya Trekking na game walk ni eneo inapofanyika, wakati game walk inafanywa ndani ya hifadhi trekking yenyewe hufanywa maeneo nje ya hifadhi na wakati mwingine kwenye vijiji vyenye makazi ya watu. Ni namna ambayo kundi hili la wageni limeamua kutembelea maeneo mbalimbali huko umasaini chini ya uratibu wa Kampuni ya Tanzania Travel ya huko Arusha. picha juu ni kundi la wageni toka nje ya nchi likiwa safarini ktk moja ya mito iliyokauka kwa ukame ndani ya bonde la Ufa.

Kushoto ni Mdau Sam Diah ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Travel akiwa na William ambae ni msimazi na mkuu wa msafara wakiwa maeneo ya Nagarrirat Swamp huko.

 Safari huwa na milima na mabonde, hapa wanapambana na kilima baada ya kulimaliza bonde. Hii ni safari ambayo itachukua siku 6 ambapo kwa siku zote hizo, wageni watakuwa wanatembelea vijiji na maeneo waliochagua kwa kutumia miguu.

Mapumziko ni muhimu ili kuweza kufikia malengo, Pichani ni mdau Sam akiwa na wageni wake wakiwa kwenye moja ya vituo walivyoamua kupumzika kwa muda wakati wa safari yao ya miguu.

Hii ni kambi iliyojengwa maalum kwa ajili ya malazi pindi jua linapozama. Kambi hizi zinajengwa na kikosi cha support cha Tanzania Travel company ambao wao wanatumia magari kuweza kuwahi kufika eneo na kuandaa camp. Hapo ilikuwa ni muda wa kifungua kinywa ktk kami ijulikanayo kama Kitumbeine.

Safari ni ndefu na kusimama kunachelewesha na kupoteza muda, hii inapelekea wadau kunywa maji kwa mrija ili kuweza kuokoa muda ili kutimiza lengo. Mmoja wa wageni wakinywa maji huku safari ikiendelea.

 Break fast


 Lunch point; Hii ni sehemu iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya maakuli ya mchana. Gari unaloliona linatumika kubebea misosi na kikosi cha kuandaa misosi na campsite. wageni hawatalipanda kwa kipindi chote cha safari yao - takriban siku 8.

Mapumziko mafupi baada ya kupata msosi kabla ya kuendelea na safari.
Shukran sana kwa Mdau Sam wa Tanzania Travel Company kwa picha hizi, picha hizi kazituma leo hii akiwa huko umasaini sambamba na kundi lake la wageni.

No comments:

Post a Comment