Monday, October 15, 2012

Jioni Moja huko Mikumi National Park hivi karibuni


Taswira toka hifadhi ya taifa ya Mikumi kama zilivyonaswa na mdau Rajab toka Wildness Safaris Tanzania hivi Karibuni. Ni picha za wanyama mbalimbali wakipata malisho yao ya mwisho kabla jua kuzama na kuelekea sehemu zao za kuegeshea mbavu zao

Swala Tomi na Nyani hupenda kutembea pamoja hususan kwenye maeneo yenye miti na vichaka. Hii ina manufaa kwa wanyama wa jamii zote mbili - Swala na Nyani. Nyani anapokuwa juu anakuwa na uwezo wa kuonda mbali na kutoa ishara kwa wengine kama hali ya usalama inaelekea kwenye dosari ktk eneo waliopo. Hii itawasaidia Swala nao kuweza kuiona hatari ikiwa mbali kabla haijawafikia. Na si hivyo tu, palipo na miti Mingi Nyani na ngedere hutupa chini maganda ya matunda walayokula juu mtini. Hii nayo huwa ni lishe kwa swala walio chini ambao kwa mazingira ya kawaida wasingeweza kuyafuata matunda/maganda hayo juu mtini.


Sio serengeti tu, Hata mikumi Nyumbu wapo japo wao hawami kama wenzao wa kule Serengeti. 

Ni Hali halisi ilivyo hivi sasa ktk hifadhi nyingi ukanda huu baada ya kipindi kirefu cha jua kali. Taarifa za kuwepo kwa mvua maeneo mbalimbali nchini zinaweza kuleta neema kwenye hifadhi zetu na kubadilisha mandhari kuwa ile kijani ya Asilia.


Jioni njiani kurudi Camp site. Wageni wengi wanaotembelea Hifadhi ya Mikumu hulala ktk hotel na camp sites zilizopo nje ya hifadhi ukiachia wachache ambao hulala kwenye camp site uijulikanayo kama Vuma Hill Tented camp site.

Poz kwa poz...
Shukran ya picha kwa Mdau Rajab na timu nzima ya Wildness Safaris Tanzania

No comments:

Post a Comment