Friday, October 26, 2012

Taswira mwanan toka Ngoitoktok - Ngorongoro crater

 Ngoitoktok ni neno la kimasai lenye kumaanisha kitu kilicho katika hali kama ya kuchemka - chemchem. Kwa Ngorongoro hilo ni jina la picnic site moja maarufu sana ndani ya crater ambapo wageni huenda kupata mlo wao wa mchana. ni sehemu iliyo pembeni ya hilo bwawa ambalo chanzo chake ni chemchem iliyopo eneo hilo hilo.


 Ni bwawa kubwa ambalo ni sehemu moja ndio wageni wanakuja kukaa na magari yao wakati upande mwingine ni kwa ajili ya wanyama nao waweza kulifikia. Tofauti na mabwawa mengine yaliyopo ndani ya crater, maji ya bwawa hili ni maji baridi (hayana chumvi).

 Si jambo la ajabu kukuta wanyama wa porini - wakali na wapole - wakisogea kunywa maji pande nyingine za bwawa hili.

Ni nyumbani kwa viboko kadhaa ambao huonekana wakiwa ndai ya bwawa mida ya mchana.

 Hawa jamaa ndio wanaowafanya wageni wa hapa wasiweze kula lunch zao nje ya magari au sehemu za wazi. Hawa ni vipanga ambao wanahusika na matukio mengi ya unyang'anyi wa vyakula kwa wageni kwenye eneo la Ngoitoktok.

kwa kawaida Vipanga huruka juu na kisha kushuka chini kwa kasi ya ajabu na kukwapua chakula au kitoweo. Siku hii hawa walikuwa wametulia tuli ardhini wakisoma mchezo. wapo wengi kwa hivyo kwa kuwaona hawa chini usidhani enao lipo shwari. wanapofanya tukio lao wanaibuka ghafla na kupotea kwa spidi ya ajabu.
                                                                            Shukran ya picha - Wildness Safaris Tanzania

No comments:

Post a Comment