Hii ndio hali halisi ambayo wafanyakazi wanaowajibika ktk hifadhi za taifa na mapori ya akiba wanakumbana nazo katika makazi yao ndani ya hifadhi zetu. Nyumba inayoonekana kwa nyuma ni moja ya nyumba ambazo wanaishi watumishi wa Idara ya wanyama pori huko Selous eneo la Matambwe. Ukipata fursa ya kuongea na mmoja wapo atakueleza kuwa hii ni hali ya kawaida ambayo wao na familia zao (zinazoishi porini) hupitia karibu kila siku aidha kwenye maeneo ya makazi (ndani ya hifadhi) au wanapokuwa wanawajibika porini. Kimsingi hapa hakuna mvamizi na kamwe hao tembo hawafukuzwi, wapo kwao.
Maeneo kama haya kukaa chini ya mti na kupunga upepo ni mwiko ambao ukikiukwa madhara yake yanaweza kuwa makubwa endapo hawa jamaa watakukuta usingizi. Maisha ndani ya hifadhi yana changamoto zake ambazo ni tofauti na maisha ya huku uraiani.
Hawa Tembo walikutwa wakiranda karibu kabisa na makazi ya wafanyakazi wa Pori la akiba la Selous, eneo la Matambwe. Matambwe ipo Upande wa mkoa wa Morogoro ambako huko ndio yalipo makao makuu na ofisi ya wahifadhi wa pori la akiba la Selous. Kwa aliyewahi panda treni ya Tazara atakuwa anakufahamu matambwe.
Shukran ya picha kwa mdau Rajab wa Wildness Safaris Tanzania
No comments:
Post a Comment