Monday, October 1, 2012

Bush Breakfast baada ya balloon flight - Serengeti


Katika utaratibu wa safari za Mapulizo ya hewa ya moto (hot Air Balloon Safaris) huko Serengeti, mgeni hupelekwa enao ambapo atahudumiwa kifungua kinywa akiwa nje porini. Kampuni ya Serengeti Balloon Safaris ina maeneo kadhaa ndani ya hifadhi ambayo imeruhusiwa kufanya shughuli hizi. Hili ni mojawapo na video hii inakuonyesha mandhari ya eneo. Kimsingi chai huandaliwa chini ya Mti mkubwa ambapo upo mita kadhaa tokea barabarani ambako magari huachwa. Hapo ni porini kabisa na nyakati nyingine wanyama husogea karibu kabisa na wanapokaa wageni kuywa chai. Kunradhi kwa kelele zinazosikika kama muugurumo, Camera iliyotumika siku hii haikuwa ktk settings zake sawasawa....
Unakaribishwa kutembelea Youtube channel ya TembeaTz kwa kubofya hapa na kujionea mkusanyiko wa video mbalimbali za mambo zilizokusanywa na timu ya Tembea Tz blog

No comments:

Post a Comment