Friday, September 14, 2012

Walking Safari - Tarangire National Park

Walking Safari ktk hifadhi na mapori ya akiba ni namna moja ambayo binafsi nakuwa naipa nafasi sana ktk mipangilio ya safari zangu za porini. Inabaki kuwa njia moja inayoniweka karibu kabisa na wanyama pori na mazingira yao katika hali ambayo ni asili na ya kipekee. Kwa hapa Tanzania, karibu hifadhi zote za taifa zinatoa fursa hii baada ya mgeni kulipia gharama husika. Mgeni husindikizwa na Ranger mwenye silaha kipindi chote cha safari, na Ranger hupanga safari kulingana na matakwa na mategemeo ya mgeni wake. Jambo la muhimu kwa mgeni ni kujiandaa na pia kufuata maelekezo ya ranger wake kipindi chote wanapokuwa porini. Jambo jingine ni kuhakikisha mnatembea kama kundi moja kipindi chote (kama mpo wengi).

Hili ni kundi la mabachelor (wote wana mapembe) wakitupisha njia na kuendelea kula.

Na wanyama (wenyeji wetu) walipigwa na butwaa kutuona tukiwa tunatembea kwa miguu wakati wao wamezoea kuwaona wageni wao wakiwa ndani ya magari

Nothing stands between you, the wildlife and the wilderness in gerenal...

Hizi sio njia za kwenda sokoni, ni mapito ya wanyama wanapokuwa wakienda kunywa maji. Kulikuwa na bwawa la maji eneo karibu na makutano haya. Nilipata wasiwasi kwani ninavyojua mimi kwenye njia kama hizi ndipo ambako Sharubu hutega mitego yake. Tulipita salama na kumaliza misele yetu salama bila ya kukutuana na sharubu, nyati au masikio kwa karibu.

Kwa karibu zaidi.

 Ulinzi kamili

Gari tuliyokuwa tukiitumia ikitufuata mimi na na Ranger ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire mahali ambapo tulikubaliana kukutana baada ya game walk. Game walk unaweza kumaliza kwa namna mbili, moja ni kurudi pale ulipoanzia au kusonga mbele na gari yako ikakufuata ndani ya hifadhi mahali na muda ambao mnakubaliana na dereva. Siku hii tulitumia option ya gari kutufuata ndani ya hifadhi, eneo lijulikanalo kama Kambi ya Simba. Ni mwendo wa takriban saa moja na nusu toka geti kuu la kuingilia hifadhi ya Taifa ya Tarangire. Baada ya hapo tulilazimika kumrudisha ranger getini ili akaendelee na majukumu yake mengine na sisi tukaendelea na program ya game drive kwa siku hiyo. Safari hizi hufanyika zaidi mida ya Asubuhi au jioni. Picha zote ni toka ktk maktaba ya TembeaTz

No comments:

Post a Comment