Friday, September 28, 2012

Uwanja wa Ndege wa Mwanza kupewa jina la Serengeti International Airport



Serengeti National Park, TembeaTz Libaray photo
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa inayoelezea kuwa Uwanja wa ndege wa Mwanza utabadilishwa jina na kuitwa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Serengeti pindi matengenezo ya uwanja yatakapokamilika. Taarfa hii iliyotolewa hivi karibuni na mmoja wa viongozi wa Serikali mkoani Mwanza. 
Watu ambao wamechangia ktk mijadala kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter wameipongeza Serikali kwa uamuzi huu ambao utaleta maboresho ktk sekta ya utalii ktk kanda ya Kaskazini. Kingine kikubwa kinachozungumzwa na wengi ni kuhusu kuinadi zaidi hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa kuupa uwanja huo jina hilo.

Ieleweke ya kwamba, kwa muda mrefu wageni wanaoenda ktk hifadhi ya Serengeti wamekuwa wakitokea au kuanzia safari zao ktk jiji la Arusha na baadhi wamekuwa wakiingia moja kwa moja kwa njia ya anga (ndege ndogo). Safari ya kutokea Arusha mjini mpaka Geti la Serengeti - Naabi hill - inachukua takriban masaa sita na nusu mpaka saba. 
kwa upande wa kutokea Mwanza mjini, safari ya kutoka Mwanza mjini hadi geti la Ndabaka inaelezewa kuchukua muda usiozidi masaa mawili - Kilometa 141. na kwa kipindi chote cha safari, barabara kati ya Mwanza mpaka geti la Ndabaka ni ya Lami. Kwa takwimu hizi, ni dhahiri uwanja wa ndege wa Mwanza (ambao muda ukifika utaitwa Uwanja wa ndege wa Serengeti) ndio uwanja mkubwa wa ndege ambao upo karibu zaidi na hifadhi ya Serengeti. 

Ramani hii toka Google Maps inaonyesha vyema kinachozungumzwa. Shukrani kwa Mdau Aenea wa Tanzania Giraffe Safaris (Arusha) kwa baadhi ya dondoo.


No comments:

Post a Comment