Tuesday, September 4, 2012

Umeshapiga kura yako??....

Chini ni ujumbe unaopata kwa njia ya barua pepe baada ya kupigia kura vivutio vinavyoshiriki ktk kinyang'anyiro cha Seven Natural Wonders of Africa.

Your votes have been received. Thank you for voting. Seven Natural Wonders is committed to helping people discover, explore and learn more about the Natural Wonders of our amazing world. Furthermore, we encourage each person to do their part in protecting these wonders. Please visit http://sevennaturalwonders.org and learn more about these wonders of nature. 

Blog ya Tembea Tanzania inazidi kuwasihi wadau wake na wale wote wanaoitakia Tanzaia mapenzi mema kupigia kura vivutio vyetu vitatu vilivyoingia kwenye mchakato SAMBAMBA na kupendekeza vingine unavyoona wewe vinafaa. Vivutio toka Tanzania vilivyoingia kwenye mtanange huu safari hii ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crater, na Migration ya wanyama ya kule Serengeti.

Dirisha la kupiga kura bado lipo wazi na ni vyema tukianza mapema kukusanya kura zetu ili kukwepa hali ya kukumbuka shuka wakati kumeshakucha. Shime wadau, inawezekana.. timiza wajibu wako.

Moderator 

No comments:

Post a Comment