Ni moja ya Alkaline lakes zilizopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Arusha. Hifadhi hii imajaaliwa kuwa maziwa kadhaa ambayo yote maji yake ni alkaline. Kwa wangi wanaotembelea hifadhi hii, Haya maziwa ni moja ya vivutio vinavyowapelekea kuitembelea hifadhi hii. Hifadhi ya Taifa ya Arusha ipo takriban kilometa 30 tokea Arusha mjini kwenye njia kuu ya Arusha - Moshi. Ipo karibu na Hoteli ya Ngurdoto. Ndani ya hifadhi hii pia inapatikana Ngurdoto crater, Crater ambayo inafanana na Ngorongoro lakini hii ni ndogo kiasi japo na yenyewe ina wanyama kadhaa ndani yake. Picha juu ni Ziwa Momella dogo kama linavyoonekana tokea kwenye gari unapolikaribia. Maziwa mengine ni Momella Kubwa na Rishateni.
hapa ni karibu kabisa na kingo za ziwa Momella dogo. Hapa ni picnic area na hivyo mgeni anaruhusiwa (kwa tahadhari) kushuka kwenye gari na kutembea kwa miguu. Kuna sehemu ya kwenda na kukaa kwa yule ambae atakuwa amebeba chakula chake na kupenda kukaa nje ya gari. Mandhari ya hapa ni tulivu sambamba na maeneo mengine yanayolizunguka ziwa hili.
Katikati ya Ziwa kuna kisiwa kama kinavyoonekana.
Ziwa hili lipo karibu na mpaka kati ya hifadhi na kijiji. Mlima unaoonekana kwa nyuma ni mlima ambao upo nje ya hifadhi na kijiji kinaitwa maji ya chai. Magari yaliyoegeshwa pembezoni mwa ziwa yapo ndani ya hifadhi na ni ya wageni wengine ambao walikuwa wanafanya Cannoe Safari ndani ya Ziwa Momella.
Mlima uliofunikwa na mawingu ni mlima Meru. Moja ya umuhimu wa Hifadhiya Taifa ya Arusha ni kwamba ndipo mahali ambapo safari za kuupanda mlima Meru zinapoanzia.
No comments:
Post a Comment