Wednesday, July 18, 2012

Sasa unaingia Hifadhi ya Taifa ya Mikumi

Kwa wengi waliopata fursa ya kusafiri kati ya mikoa ya Iringa na Morogoro watakuwa wanafahamu fika maeneo haya. Hapa ni geti ambalo lina lengo la kumtahadharisha msafiri kuwa sasa anaingia eneo la hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Ni barabara yenye urefu wa takriban kilometa 50 ambazo zinakatisha kwenye hii hifadhi.

Licha ya tahadhari na maelezo yote, matukio ya ajali za wanyama kugongwa na uchafuzi wa mazingira ndani ya hifadhi unaofanywa na wasafiri yanazidi kukithiri. Hali ya uchafu ndio inaonekana ki urahisi pembezoni mwa barabara hii ambapo wasafiri wamekuwa wakitupa takataka bila kujali ndani ya eneo la hifadhi. Hii si salama kwani inahatarisha maisha ya wanyama. Makopo ya soda, chupa za maji ya kunywa zilizotumika sambamba na alminium foil zilizofungiwa chakula zinaonekana kirahisi pembezoni hususan mida ya jioni. Hali hii inahitaji juhudi za pamoja ili kuwanusuru wanyama wanaohifadhiwa.

Hali unayoiona Mikumi ni tofauti sana na Hifadhi nyingine ambazo hazina barabara zinazokatisha katikati. Wengi wa guides wanaopeleka wageni kwenye hizi hifadhi huwa mstari wa mbele ktk kuwaelemisha wageni wao kuhusu utunzaji wa mazingira na kuhakikisha kuwa wageni hao wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa ktk hifadhi husika. Kwa hili nawapongeza waongoza wageni kwa kuwa mastari wa mbele kwenye utunzaji wa mazingira na kuwalinda wanyama ndani ya hifadhi. 

Uwepo wa hawa jamaa pembezoni mwa barabara hii na hata nje ya hifadhi inatokana na kushamiri kwa vitendo vya utupwaji takataka ovyo vinavyofanywa na wasafiri. kuanzia Mikumi mpaka Milima ya Iyovi na Kitonga, hawa jamaa wanakuwa wengi hususan mida ya mchana wakisubiri makombo yanayotupwa na wapita njia.

No comments:

Post a Comment