Friday, June 8, 2012

Mhe Nyalandu Azindua Maonesho ya Karibu leo

Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu leo mchana amezindua rasmi maonesha makubwa ya sekta ya Utalii ya Karibu mjini Arusha. Baada ya kuwasili ktk viwanja vya Maonesho Mhe Nyalandu alipata wasaha wa kuzungumza na viongozi wa TTB, TATO sambamba na waandaji wa karibu fair. Picha juu ni Mhe Nyalandu akiteta jambo na mwenyekiti wa shirikisho la tour operators Tanzania, Mhe Mustapha Akunaay (kulia). Wengine ni  Sam Diah mmoja wa waratibu wa maonesho sambamba na Bi Devota Mdachi, Mkurugenzi wa Masoko wa TTB.   

 Mazungumzo yakiendelea ndani ya Banda ambalo taasisi kadhaa za Serikali zenye dhamana ya utalii zimepiga kambi kwenye maonesho haya ya Karibu.

 Mhe Nyalandu akipokea zawadi toka kwa Mkurugenzi wa masoko wa TTB Bi Devotha Mdachi baada ya mazungumzo mafupi ktk banda la taasisi mbalimbali za serikali zenye dhamana ya Utalii.

Akipata maelezo kwenye banda la Cultural tourism programmme

Ktk banda la Precision.

 Akipata maelezo ya kampuni inayotoa huduma za helikpta hapa Tanzania ya Whirlwind. Anayempa Maelezo ni Capt. Neels. Ktk Maelezo yake, Capt Neels alisema kuwa kampuni yake ipo mbioni kuleta helikopta tano mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Mpango wao ni kuzitawanya maeneo mbalimbali ya nchi hii ili ziweze kutumika kwenye huduma za dharura haraka pale zinapohitajika. Sasa hivi wana helikopta moja nchini.
Akiendelea kutembelea mabanda mbalimbali ktk maonesho.

No comments:

Post a Comment