Thursday, June 21, 2012

Kilimanjaro International Airport hivi Karibuni

Ni miaka takribani 22 imepita tokea nipite kwenye huu uwanja kama msafiri. Hivi majuzi nilipata fursa ya kupita hapo nikitokea Arusha kurudi Dar. Muda niliokaa hapo uwanjani ulivuta na kurudisha kumbukumbu nyingi sana binafsi za enzi hizo. Picha hizi ni baadhi ya picha nilizoweza kupiga nikiwa hapo. katika kipindi kirefu kwa hivi karibuni, safari zangu za Arusha zilikuwa ni kwa njia ya Barabara. Uwanja huu wa ndege ni kiungo muhimu sana kwa sekta ya Utalii hususan kwa vivutio vilivyopo ktk Ukanda wa utalii wa Kaskazini. japo miaka mingi imepita, bado muonekano wa uwanja umebaki vile vile hali ambayo ilichangia sana mimi kuweza kuvuta taswira niliyoihifadhi ya uwanja huu ulivyokuwa enzi hizo.

Kushoto ni sehemu kwa ajili ya wageni wanaowasili na upande wa kulia ni sehemu kwa ajili ya wageni wanaoondoka.

Mchuma wa Precision Air (ATR 72) ukiwa umeweka pozi kusubiri kupakia Abiria. Safari za Ndege hizi kutokea Arusha kuja Dar hupitia ZNZ. Hii ruti ni muhimu kwa sekta ya utalii kwani kwa wageni wengi wanaotoka nje huanza kwanza kwa kufanya safari za maporini na sehemu nyinginezo na mwisho huelekea ZNZ kwa mapumziko kwenye pwani kabla ya kukwea mapipa kurudi makwao. Huu ndio umekuwa mpango wa safari kwa wageni wanaokuja Tanzania hususan wale ambao hununua package za beach holiday. Siku hii karibu robo tatu ya abiria wa ndege hii walikuwa ni wageni toka Denmark ambao walikuwa wametokea Ngorongoro na wote walishuka Zanzibar kuendelea na mapumziko.

Moja ya mambo ambayo Mhe Nyalandu alipewa kama lalamiko na wadau wa utalii ktk Karibu fair ni mpango wa ruti ambao ATCL inautumia. Abiria wanaotoka Arusha kuja Dar Hupitishwa kwanza Mwanza na kisha wanaletwa Dar. Baadhi ya wadau walitoa lalamiko hilo ambao na wao walilipata toka kwa wageni wao.

No comments:

Post a Comment