Tuesday, June 12, 2012

Asubuhi moja huko Maramboi Tented Camp; Tarangire - Lake Manyara

 Maramboi Tented camp Lake Manyara
Maramboi Tented camp ni moja ya hoteli zinazomilikiwa na kampuni ya Tanganyika Wilderness camps. Hoteli hii ipo katika ushirobo wa wanyama (wildlife corridor) uliopo  kati ya hifadhi za Manyara na Tarangira huko Arusha. Japo yenyewe imejengwa karibu na ziwa Manyara, lakini haipo ndani ya eneo la hifadhi ya Manyara. Jicho la blog ya Tembea Tanzania lilipata fursa ya kupiga kambi katika hoteli hii mwezi Julai mwaka 2010 na mtundiko huu unakuletea picha zilizopigwa asubuhi moja zikionyesha mandhari ya eneo la hoteli sambamba na mazingira yake muda wa asubuhi. Picha juu ni Nyumbu ambao walikuwa wanakula nyasi karibu na hema ambalo timu ya Tembea Tanzania ilikuwa limelala usiku wa kuamkia siku hii. Kwa nyuma ni ziwa Manyara na mlima unaoonekana kwa mbali ni kingo za Bonde la ufa. Eneo hili lipo ndani ya bonde la ufa.

 Maramboi Tented camp Lake Manyara
Hawa nyumbu walikuwa wapo  karibu kabisa na hema kuu la kupata mlo na kifungua kinywa

 Maramboi Tented camp Lake Manyara
 Ina bwawa la kuogelea ambalo linatoa mandhari nzuri ya ziwa Manyara sambamba na kingo za Bonde la Ufa
 Maramboi Tented camp Lake Manyara
Ziwa manyara likionekana kwa mbali

 Maramboi Tented camp Lake Manyara

 Maramboi Tented camp Lake Manyara


 Maramboi Tented camp Lake Manyara

 Maramboi Tented camp Lake Manyara
Muonekano wa eneo la kati ya hoteli na ziwa Manyara tokea kwenye hema la kulala
 
 Maramboi Tented camp Lake Manyara

 Maramboi Tented camp Lake Manyara
Kuna bwawa la maji kwa ajili ya wanyama. Punda hawa walikuwa wanaelekea kwenye bwawa hilo sambamba na nyumbu waliokuwa wameongozana nao. Pata picha zaidi kwenye tovuti ya hoteli kwa kubofya hapa

No comments:

Post a Comment