Thursday, May 24, 2012

Taswira za Serengeti NP aka Shambani.

 Ukimsikia Mdau wa sekta ya utalii akisema ameenda Shambani basi ujue huyo atakuwa ameenda hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Picha hizi zinajieleza waziwazi kwanini Serengeti imepewa jina la Shambani. Ngorongoro crater huitwa shimoni

 Haya ni maeneo Kusini mwa Serengeti NP ukiwa unaelekea kwenye geti la Naabi - Kama unatoka nje ya Serengeti kwenda Ngorongoro.
 Hawa nyumbu walipiga stop ya migration yao kuelekea kusini baada ya kukutana na sharubu (picha chini). Kundi lote hili lilisitisha migration kwa kumhofia sharubu mmoja.
Hapa kulikuwa na Sharubu dume ambaye aliwafanya nyumbu waliokuwa kwenye migration wasimame kwa muda. Ama kweli mfalme ni mfalme, hata akiwa wa porini huheshimiwa. (Picha zote toka Makataba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment