Friday, May 25, 2012

Oldupai Gorge

Sio kwamba nimechapia, bali hilo ndio jina sahihi la hili eneo ambako kulikutwa mabaki na vifaa mbalimbali vya mwanadamu wa awali aliyepata kutembea kwa miguu miwili. Kimsingi jina la eneo hili linatokana na neno la kimasai la "Oldupai" neno hili maana yake ni katani mwitu. Huu mmea wa katani mwitu (kama Aloe vera flani hivi) unapatikana kwa wingi sana eneo hili. Wataalamu wa mambo ya kale baada ya kugundua mabaki walioyaona, walilazimika kulipa jina eneo hilo la kihistoria ili liingizwe katika taarifa. Wakaamua kulipa jina la asili. Mjerumani (Wilhelm Kattwinkel) ambae alikuwa wa kwanza kulibaini eneo hili alipokuwa akiandika jina alilotamkiwa, akaandika Olduvai badala ya Oldupai kama inavyotakiwa kimasai - lugha gongana. Jina hilo (ambalo silo sahihi) likaenda mbele na mbali kiasi cha kufanya lionekane ni kama jina sahihi. Yawezekana likaonekana ni jina sahihi lakini kimantiki, linapashwa liwe Oldupai - ili kumaanisha katani mwitu inayopatikana kwa wingi maeneo haya. Kuanzia mwaka 2005, eneo hili likaanza kutumia rasmi jina lake sahihi la Oldupai japo bado wapo ambao wanaendelea kutumia lile jina la zamani.

makala hizi mbili toka Wikipedia zinaweza kukupa mwanga zaidi;
(picha toka Maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment