Tuesday, May 29, 2012

Taswira za hivi karibuni toka Ngorongoro Crater

 Wadau waliokuwa safarini huko Ngorongoro Crater chini ya usimamizi wa Timu ya RA Safaris walikutana na sharubu hawa wakiwa 'bize'.

 Ukiwa porini na ukawasikia madereva na tour guides wanazungumzia habari ya sharubu kwenda Harusini basi ujiandae kukutana na mambo kama haya.

 Ni Mkao wa ki-usalama zaidi. Hapo kila mmoja anamchunga mwenzie na kuwa tayari kutoa ishara kwa kundi endapo adui ataonekana. Unapokutana na kundi la pundamilia au hata wanyama wengine wala nyasi, mara nyingi utakuta kuna baadhi yao ambao hawajishughulishi kutafuta au kula nyasi. Wanakuwa wameachiwa lindo ili kuwachunga wenzao. Huu ni moja ya mkao wanaopenda kuutumia pundamilia ili kuweza kumuona adui yao kokote atakapotokea.

Wadau wa RA safaris wakiwa na wageni wao. Hapa wakiwa njiani kuelekea Serengeti. 
Picha kwa hisani ya mdau Zeph wa RA Safaris

No comments:

Post a Comment