Tuesday, May 29, 2012

Mambo ya Arusha National Park

Kwa mtizamo wangu binafsi, Arusha National Park ni moja ya hifadhi za taifa ambazo zipo karibu kabisa na moja ya miji mikubwa hapa Tanzania. Takriban Kilometa 25 tokea Arusha Mjini. Ni hifadhi ambayo ina upekee wa namna yake kama ambavyo zilivyo hifadhi nyingine za hapa nyumbani. Ni hifadhi ambayo mgeni anapata fursa ya kufanya shughuli mbalimbali kama vile walking safari, camping, Game drive na pia ndipo safari za kupanda Mlima Meru zinapoanzia. Kama mdau utakuwa umetembelea Jiji la Arusha na kujikuta una nafasi ya mapumziko, usisite kufanya mpango wa kuitembelea hifadhi hii na kujionea mandhari nzuri iliyohifadhiwa sambamba na wanyama kedekede wa porini. Picha juu ni wageni wa Kamuni ya RA Safaris ambao walitembelea hifadhi hii hivi karibuni. Picha kwa hisani ya Mdau Zeph wa RA Safaris

No comments:

Post a Comment