Friday, March 23, 2012

TTB yapata bodi mpya

Mhe. Maige ATEUA BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel M. Maige (MB) kwa Mamlaka aliyonayo

amewateua wajumbe watano kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii (TTB)

kuanzia tarehe 23 Machi, 2012.

Uteuzi huo unafuatia Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete kumteua Balozi Charles A. Sanga

kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTB mapema wiki hii. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa

Bodi hiyo itakayodumu kwa miaka mitatu ni pamoja na:-

1. Prof. Isaya Jairo PhD, Mhadhiri wa Biashara na Uchumi, Chuo cha Usimamizi wa
Fedha, IFM;

2. Ndugu Teddy Mapunda, Mtaalamu wa Masoko (Marketing) na Afisa Uhusiano
Serengeti Breweries Limited;

3. Ndugu Samwel D.I. Diah, Mtaalamu na Mdau wa Biashara na Utalii na
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Travel Co. Limited;

4. Mhe. Kaika S. Telele (Mb), Mbunge wa Ngorongoro na Mdau wa Utalii na;

5. Mhe. Abdulkarim Shah (Mb), Mbunge wa Mafia na Mdau wa Utalii.

(chanzo - MjengwaBlog)

-----------

Blog ya Tembea Tanzania inawapongeza wote walioteuliwa na kuwatakia kila la kheri katika kutekeleza vyema majukumu yao. Pia kwa Nafasi ya pekee blog ya TembeaTz inachukua fursa hii kumpongeza Mdau wake Samwel Diah kwa kuteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya TTB.

Bofya hapa kusikia Mazungumzo baina ya Mdau Sam Diah na Mhe Lazaro Nyalandu wakati wa uzinduzi wa Karibu Fair 2011, Arusha mwezi June mwaka Jana. Hapa alikuwa akizungumza kama Mkurugenzi wa Tanzania Travel Company Ltd

No comments:

Post a Comment