Friday, March 23, 2012

Safari ya kwenda kisiwa cha Mbudya, Dar Es Salaam

Vibanda vya kupumzikia wageni na pwani yenye mchanga mweupe kwenye Kisiwa cha Mbudya vikionekana vyema tokea kwenye boti.

Sehemu ya Kusini mwa kisiwa cha Mbudya inavyoonekana tokea mbali.

Siku hii tulikuwa na raia wengine wengi wa kutoka mataifa ya nje ambao wanaishi na kufanya kazi hapa Dar/Tanzania. Baadhi yao walionekana kuyafahamu vyema mazingira na mambo ya kisiwa hiki.


Hapa ni baada ya kutia maguu ndani ya kisiwa. Kisiwa hiki ina sehemu mbili kuu za kupumzikia. Kuna upande hii wa Magharibi wa Kisiwa ambao mgeni akisimama anakuwa anaona maeneo ya Kunduchi. Eneo hili hujulikana kama beach 1. Eneo jingine lipo Mashariki mwa kisiwa ambako huko kunafahamika kama Beach 2. Ni mwendo wa takriban dakika 20 hivi toka beach 1 kwenda beach 2 kwa miguu ndani ya kisiwa.
(picha - maktaba ya TembeaTz)

No comments:

Post a Comment