Thursday, March 15, 2012

Mkao wa Timing huu....

Hawa Sahrubu walikuwa wamekaa katika mkao ambo ulimfanya Mdau Tom na wenzake kupata shauku ya kujua kifuatacho "ITV"... Sharubu hana ubavu wa kukimbia kwa muda mrefu iwe kwa mwendo wa kasi au taratibu. Hivyo mawindo yake daima hutegemea sana timing ambapo huruhusu windo liingie ndani ya 18 zake ndio kisha aanze kumshambulia na kumwangusha. hii humpunguzia safari ya kukimbia na kumhakikishia kuongeza nafasi ya kupanda mawindo kila pale anapoamua. Kikubwa kwa Sharubu ni kwamba anayewinda ni Sahrubu jike. Hata ukiangalia picha juu utaona wote ni masharubu jike na watoto. Dume hapo linakuwa lipo mbali likipumzika na kusubiri windo liende poa na kisha yeye kuja kula. Sharubu dume sio mwindaji na hata akiamua kuwinda, hutegemea zaidi bahati. Ujanja na uwezo wa kuwinda wanao majike. Dume ni mzee wa boma, jukumu lake kubwa ni ulinzi wa majike na watoto wao dhidi ya madume wengine (wavamizi).
Ukitizama picha utabaini ya kuwa kuna baadhi ya sharubu ambao wameangalia upande mmoja kwa umakini mkubwa. Hii ni ishara tosha kwamba huko kuna mnyama ambae wanamfanyia timing wakisubiri aingie kwenye 18 zao. na kwa tukio hili, alikuwa ni nyati dume aliyekuwa mita chache tokea hapo walipo hawa sharubu. Kwa bahati mbaya au nzuri, jaribio hili halikwenda sawia ambapo mtego wao ulishindwa kuzaa matunda.
(Picha na mdau Tom wa Kima Adventures)

No comments:

Post a Comment