Tuesday, January 31, 2012

Wanapolala swala dume...

Tulipokuwa kwenye game walk ktk pori la akiba la Selous, tulifika mahali tutakuta lundo la mboji ya swala. guide alitueleza kuwa hiyo ni shughuli ya swala dume.
Alifafanua ya kwamba swala dume hulala kwenye kundi moja huku wote wakiwa wanapeana migongo na kutengeneza kitu kama mduara. vichwa huwa nje ya mduara vikiangalia kila pembe ya pale walipo. Hii ni mbinu yao ya usalama ili kuhakikisha kuwa adui ataweza kuonekana toka upande wowote. Wakati madume wakilala pamoja, majike huwa wanakuwa wametanyika sehemu nyingine ambako huwa pamoja na watoto (kama wapo). Kipindi chote cha usiku, swala madume ndio huwa wanaacha alama ya hiyo mboji kwani humaliza shughuli zote hapo hapo wanakuwa lindoni. Tulikutana na mizigo kama mitatu ya shehena za mboji hii ktk eneo hili wakati wa mizunguko yetu kwa miguu.

No comments:

Post a Comment