Thursday, January 26, 2012

Mdau Aukwea Mlima Meru hivi karibuni

Tembea Tanzania
Ni John Kessy wa Moshi, mmoja wa maveteran wa blog ya Tembea Tanzania ambae hivi karibuni alipanda Mlima Meru akiwa sambamba na kundi la wanafunzi tokea chuo kikuu kimoja cha nchini Marekani. wanafunzi hawa wapo nchini kwa mafunzo ya vitendo ktk nyanja mbalimbali na mdau John ndio mwenyeji wao. safari ya kupanda Mlima Meru huanzia katika hifadhi ya taifa ya Arusha, kwenye Geti la Momella. Picha juu ni mdau akiwa kwenye moja ya maporomoko madogo ya maji yaliyopo ndani ya hifadhi ya Arusha wakati wa kuanza safari ya kuupanda mlima Meru.

Tembea Tanzania
safari ikiendelea. Hapa wakiwa wanaelekea ukingoni mwa hifadhi ya taifa ya Arusha.
Mlima meru ni sehemu ya hifadhi ya taifa ya Arusha

Hapa ni katika kituo kijulikanacho kama Saddle hut. Kituo kingine hujulikana kama Miriakamba.
Tembea Tanzania
Mwendo wa takriban masaa mawili toka Saddle hut utakufika mahali hapa ambapo wageni huenda kwa lengo la kuuzoesha mwili - acclamatisation; panaitwa Little Meru. Hiki ni moja ya vilele viwili vya Mlima Meru.

Tembea Tanzania
Ni sehemu ya mizunguko kwa ajili ya kuuzoesha mwili na mazingira ya juu mlimani kabla ya kuzidi kusonga mbele ambako kiwango cha oksijeni kwenye hewa huwa kinapungua tofauti na mazoea

Meru ni Mlima ambao umetokana na milipuko ya lava/volcano iliyotokea miaka mingi iliyopita. Picha juu ni moja ya kumbukumbu ya sehemu ambazo Lava ilikuwa inachomokea. Hii sehemu inaitwa Ash cone.

Hapa ni kuelekea kwenye kilele chenyewe cha Mlima Meru. Kinajulikana kama Big Meru

Big Meru

baada ya kushuka Mlimani na hapa wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha wakielekea Geti la Momella. wageni wanaopanda mlima wanapokuwa ndani ya hifadhi husindikizwa na ranger kwa ajili ya usalama wao mpaka wanapofika eneo lenye mwinuko mkali ambako wanyama wakubwa na wakali hawafiki.

Hawa walikuwa mita kadhaa tokea njiani kuelekea geti la Momella
Shukran kwa mdau John Kessy kwa picha na taarifa.

No comments:

Post a Comment