Thursday, December 1, 2011

Wote huweka alama, lakini zinakuwa ni tofauti kidogo

Viboko Dume hutawanya kinyesi chao kwa mkia ktk eneo ambalo anaweka alama yake ya kufuata anaporudi bwawani.

Kiboko jike huweka alama, lakini kwakuwa yeye sio mmiliki wa eneo alama zake huwa anazishora chini. Huwa hatapanyi kwa mkia kama vile ambavyo dume anafanya. ktk picha mbili hizi utaona kuna aina moja ya 'mzigo' umetupwa chini wakati mwingine umerushwa mpaka kwenye matawi ya mti ulio pembeni. Ni baadhi ya mambo unayoweza kujionea kwa ukaribu na kujifunza unapoamua kufanya game walk safari.

2 comments:

  1. asante sana kwakutujuza mambo ya wanyama unafanya vizuri sana ambao tulikuwa hatuelewi mambo ya wanyama tunajifunza mengi ubarikiwe sana endelea kutujuza zaidi na zaidi big up

    ReplyDelete
  2. Anony wa kwanza, nashukuru kwa ujumbe wako. Ni wadau kama ninyi mnaonipa moyo wa kuendelea na hiki ninachokifanya kupitia blog hii siku hadi siku.
    Nashukuru sana na nitajitahidi kuendeleza libeneke la Tembea Tanzania licha ya changamoto zake zilizopo.

    Siku njema.

    KK

    ReplyDelete