Thursday, December 1, 2011

Usisimame mbele ya shimo.......

Ni moja ya mambo ambayo nilijifunza wakati wa game walk huko pori la akiba la Selous. Ukifika mahali ukakuta kuna shimo la mnyama, ni vyema ukilisogelea (ikibidi) kwa usawa wa pembeni na mlango wa shimo hilo. Hii itakusaidia endapo mwenye nyumba ataamua kutoka ghafla na kukukuta wewe ukiwa umesimama au unatembea usawa wa mlango wake.

Wanyama ambao wanaelezwa kuongoza kwa mashambulizi ya namna hii ni bwana afya au ngiri. wanapohisi uvamizi hutoka nje kwa spidi ya ajabu usawa wa mlango bila ya hata kuangalia vyema. picha zote mbili ni guide tuliyekuwa nae akilikaribia shimo hili kwa pembeni. Licha ishara zote kuonyesha kuwa shimo hilo halijatembelewa muda mrefu lakini tahadhari kama hizi ni muhimu kuzichukua. Fisi na ngiri wao pia huvamia mashimo yaliyoachwa na mhanga mnyama ambae anafahamika kwa kuchimba mashimo makubwa na hata kwa kuharibu vichuguu vya mchwa.

No comments:

Post a Comment