Monday, December 12, 2011

Ni Campsite kila hatua, Mloka - Selous

Unapoanza kukiacha kijiji cha Mloka na kisha kuelekea lilipo geti la Kuingilia Selous (mtemere) utaanza kukutana a vibao vikikuonyesha zilizopo campsite kadhaa. Campsite nyingi za Mloka zimejengwa pembezoni mwa mto Rufiji. Ukiwa unaelekea Mtemere nyingi zipo upande wa Kushoto wa barabara. Picha hizi zilipigwa tukiwa tunatoka Geti la Mtemere kurudi campsite tuliyokuwa tumefikia.

Wilderness camp ipo upande wa pili wa mto Rufiji. kibao hiki kinawaelekeza wageni waweze kufika eneo ambalo watapandia boti na kuvuka mto ili kufika ilipo campsite.Kushoto ni njia inayoelekea Geti la Mtemere. Njia iliyonyooka ni njia ambayo inaenda kuibukia Kisarawe. Ni njia ambayo hutumiwa na watu wachache na nilielezwa ya kuwa wawindaji wanaokuja kwa magari ndio huwa wanaitumia mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment