Friday, November 18, 2011

Njiani kuelekea Mbuyu mkubwa - Selous

Bila ya dondoo yoyte tulibahatika kuwakuta sahrubu jike wawili wakiwa wamepumzika chini ya mti eneo karibu na ziwa Manze. Hapa tulikuwa njiani kuelekea kwenye Mbuyu unaosemekana kuwa mkubwa kuliko yote na wenye umri mkubwa ndani ya pori la akiba la Selous. Kwa jinsi walivyokuwa wamelala na eneo lao, ni dhahiri wageni wengi hawakuwaona hawa sharubu.

Tulikutana na gari moja ya wageni mita chache kabla ya kuwaona hawa sharubu na dereva wao hakuwazungumzia kabisa. Awali walikuwa wamekaa mbalimbali lakini baadae mmoja alihama toka upande mmoja na kumfuata mwenzie upande wa pili.

No comments:

Post a Comment