Friday, November 18, 2011

Lunch at Mbuyu Mkubwa - Selous GR

Ukisikia mtu alipata lunch yake Mbuyu Mkubwa akiwa pori la akiba la Selous basi elewa alipata chakula ktk maeneo ya mbuyu unaoona ktk picha juu. Ni mbuyu ambao unasemekana kuwa una umri mkubwa ukilinganisha na mibuyu mingine. Baada ya kukosa nafasi ktk ule mti wa Lake Manze, tuliamua kuja kutulizana chini ya mbuyu mkubwa na kupata msosi wetu hapa. Picha juu ni gari la wageni waliokuwa wametutangulia ambao walikuwa wakianza kuondoka na kutupisha

Ndinga yetu ikiwa imepozi chini ya Mbuyu mkubwa. Mbuyu huu upo eneo ambalo lipo karibu na Ziwa Manze. Mdau Bavon (shoto, aliyekaa) na Mdau Tom wa Kima Safaris (kulia) wakiendelea kupata maakuli. Mlango wa ndinga tuliuacha wazi 'just-in-case'.....


Eneo karibu na mbuyu mkubwa

Sehemu nyingine kuna uwazi mkubwa unaotoa mandhari murua ya eneo hili.

1 comment:

  1. Nimeipenda blog yako bro imenipa hamasa yakufanya utalii nyumbani, keep up! says Twaha from Moscow

    ReplyDelete