Ni Kundi ambalo himaya yake ni sehemu kubwa ya eneo linalozunguka ziwa Manze. Ni kundi lenye simba wengi ambao hutapakaa sehemu kubwa ya ukanda wa ziwa Manze. Hapa tuliwakuta wakiwa pembezoni kabisa mwa barabara iendayo Matambwe. ilikuwa vigumu kupata idadi yao kamili lakini lilikuwa ni kundi lenye sharubu jike na watoto kadhaa. Ilikuwa kama bahati kuonana nao kwani hatukutegemea kuona sharubu maeneo haya ya wazi na kame hivi
Rangi yao ilishabihiana na rangi ya mazingira ndio maana nasema ilikuwa ni kama bahati kuweza kuwaona. Nadhani wangi waliotutangulia waliwapita bila kuweza kuwaona kutokana na jinsi walivyokuwa wamekaa hapo.
No comments:
Post a Comment