Tuesday, October 25, 2011

Toka Kibiti kuelekea Mloka

Safari ya kutoka Kibiti kuelekea Kijiji cha Mloka (kijiji cha mwisho kabla ya kuingia Selous) huwa ni ya umbali wa kilometa 100. Hatua ya kwanza huwa ni kutoka Kibiti mpaka eneo lijulikanalo kama Mkongo. Hapo kuna Njia panda ya kuelekea Mloka, Ikwiriri na maeneo mengine ya Utete. Kibiti - Mloka ni Kilometa 20. Picha ya juu niliipiga kilometa kadhaa baada ya kuachana na eneo la Kibiti Njia Panda.

Sehemu kubwa ya safari inakuwa ni ya kukatisha maporini japo baada ya kilometa kadhaa kunakuwa na kijiji au eneo la makazi. Mvua zilizonyesha hivi karibu zimebadilisha mandhari ya maeneo mengi ya huku na kuyapa rangi ya kijana.

Ndinga ya Safari.

Hapa ndio njia panda ya Mkongo. Barabara inayoelekea Kulia ndiyo itakayokufikisha Mloka na maeneo mengineyo ya njiani. Ya Kushoto itakupeleka Ikwiriri.Ukinyoosha moja kwa moja utakuwa unaelekea maeneo mengine huko Utete. Kwa wale ambao wataamulia kuachana na barabara ya Lami na kuanzia safari yao Ikwiriri watakuja kuibukia barabara ya kushoto. wengi wa wale wanaoanzia safari Ikwirir wengi huwa ni wale wanaoenda kuliona daraja la Mkapa ambalo lipo kilometa chache toka Ikwiriri "mjini". Kutoka hapa mpaka Mloka ni umbali wa Kilometa 80 na kuifanya safari toka Kibiti mpaka Mloka kuwa ya kilometa 100.

Uwepo wa mchanga pembezoni mwa barabara ni ushahidi wa barabara hii kufanyiwa usawazishwaji hivi karibuni.

Safari ikiendelea. Safari ya Kutoka Kibiti mpaka Mloka itakupitisha kwenye vijiji takriban 11 vilivyo pembezoni mwa Barabara hii.

No comments:

Post a Comment