Ni katika barabara ya kutoka Bagamoyo kuelekea msata. Barabara hii ina umbali wa kilometa 64 na tayari kuna sehemu (takriban kilometa 20 hivi) mkeka umeshatandikwa na mkandarasi. Eneo hili lenye mkeka lipo karibu na Msata ukiwa unatokea bagamoyo. Picha juu ni mwanzoni mwa eneo lilipigwa mkeka tayari, karibu na kambi ya mkandarasi.
Mkandarasi anayeijenga barabara hii kwa sasa ni mkandarasi wa pili baada ya yule wa awali kuchemsha na kufungishwa virago.
Naona sasa njia zimekuwa nzuri na kurahisisha usafiri kwa wasafiri wa hizo njia!
ReplyDeleteIla kuna sehemu nyingine pia inabidi ziangaliwe maana kuna njia mbovu tu!
dah dafi sana,hapa kodi za watanzania zimetumika kiuhalali.
ReplyDeleteni kweli kodi za wananchi wa mbinga zimetumika vyema kujenga barabara za bagamoyo ambao kazi yao kubwa ni kucheza bao. huko mbinga watu wanadunda kwenye tope kama kawa, yaani wanasafirisha kahawa kwa siku mbili katika umbali wa kilometa 15
ReplyDeletebarabara nzuri sana! Kazi njuri
ReplyDelete