Sunday, September 4, 2011

Wa chini na Windo lake... Serengeti NP

Duma "wa Chini" akiwa na windo lake la swala tomi (Thomson's gazelle) ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti.



wa chini yeye humalizia shughuli yote ardhini. Hana ubavu wa kupandisha windo lake juu ya mti kama afanyavyo wa juu. Ili kukwepa kuporwa windo lake na fisi au simba wa chini hulazimika kula windo lake fasta kabla hajashtukiwa na kuletewa zengwe na hao watajwa. Kutokana na kuwa na mwili mdogo mdogo, wa chini hana ubavu wa kupambana na bwana afya au sharubu.

Uwepo wa pembe kweny kichwa cha swala Tomi huyo kunadhihirisha ya kwamba alikuwa ni swala dume.
Hapo wa chini huyu anaweza hesabika kama kafanya uwindaji ambao unazingatia uhifadhi. ktk ugawaji wa vibali vya kuwinda, mwindaji hupewa kibali cha kuwinda mnyama dume. muwindaji hulazimika kuhakikisha kuwa anawinda mnyama dume kama taratibu zinavyoelekeza. Sababu moja inayopelekea uwepo wa taratibu hii ni kukwepa kuwinda majike ambayo yanalea watoto na kuweka hatarini kikazi cha jamii ile. Au hata kukwepa kuwinda mnyama aliye na uja uzito na kupelekea kuwinda idadi kubwa ya wanyama zaidi ya kibali ulichopewa, ukijumuisha na wale watakaokuwamo tumboni mwa jike. Picha na Mdau Tom wa Kima Safaris

No comments:

Post a Comment