ni Moja ya makundi ya sharubu maarufu ndani ya pori la akiba la Selous. Utakapotembelea Selous GR unaweza bahatika kuliona likiwa mapumzikoni kama alivyolikuta mdau Stephen wa Kima Safaris au ukalikuta limeangusha mnyama. Ni wawindaji hodari
Wengi walijumuika kuliangalia kwa karibu the siwandu pride. Hapa ndipo unapoona tofauti kati ya kutembelea hifadhi ya taifa na pori la akiba. Kwenye hifadhi ya taifa hairuhusiwi kuendesha gari nje ya barabara zilizopangwa na wahifadhi. kwenye mapori ya akiba, ni ruhusa kwa wageni kupeleka gari popote pale ili kuweza kumuona mnyama au kitu kwa karibu. Siku hii, sharubu hawa walikuwa wamekaa mbali na barabara. kwakuwa wazoefu wa Selous wanajua vijiwe vya pride hii, huwafuata (nje ya barabara) ili kuweza kuwaona kwa karibu. Hii ingetokea ktk hifadhi, basi wadau hawa wangeishia kuwaangalia kwa mbali. Picha na mdau Stephen wa Kima Safaris
No comments:
Post a Comment