Sunday, August 28, 2011

Pembezoni mwa ziwa Mzizimia one - Selous GR

Ndani ya pori la akiba la Selous kuna 'maziwa' mengi ambayo yanatengenezwa na mto rufiji. Kimsingi haya ni ox-bow lakes ambayo huonekana kirahisi pale maji ya mto Rufiji. Maji yakiongezeka kina maziwa haya huwa sehemu ya mto rufiji. Mtundiko huu ni taswira zilikusanywa na mdau Stephen pembezoni mwa mojawapo ya maziwa hayo lijulikanalo kama Mzizimia One. Mazwia mengine ni Mzizimia 2, Siwandu, Nzelakela, Tagalala na mengineyo.




Njaa inapomzidia, kiboko hutoka nje ya bwawa hata mchana ili kuweza kupata chakula cha kujikimu. Mara nyingi, hawa jamaa hutoka nje ya mabwawa yao mida ya usiku na kutafuta nyasi nchi kavu. Mchana wanapotoka huwa hawachezi mbali na bwawa lao kwani ndio nyumbani kwao na ni mahali ambako wana uhakika wa usalama wao. Mida ya usiku huwa wanaenda mbali na mabwawa au mito ili kujitafutia chakula. Kingine kinachowazuia kwenda mbali ni ngozi yao isiyokuwa na uwezo wa kustahimili jua kali. Baada ya muda hulazimika kurudi majini ili kupunguza makali ya miale ya jua kwenye ngozi na mwili wake.

Huyu alikuwa akiendelea kutafuta chochote pembezoni ya ziwa mahali ambako kulikuwa na kivuli. Picha zote na Mdau Stephen wa Kima Safaris aliyekuwa Selous hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment