Sunday, July 24, 2011

Serengeti NP

Ilikuwa ni Alfajiri na mapema ambapo timu ya TembeaTz ilikuwa eneo la Maasai Kopjes ikisubiri kuanza kwa safari ya Balloon ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Ratiba ya kufika eneo la kurukia mapema ilipelekea sisi kushuhudia jua likichomoza na kuona wanyama wakianza kuamka na kuanza mizunguko yao. Wale waliokuwa na misele usiku kucha, tulibahatika kuwaona nao wakitafuta sehemu za kutuliza vichwa vyao.

No comments:

Post a Comment