Monday, July 4, 2011

Ngurumo zake...

katika jamii ya sharubu, ni sharubu dume ndie mwenye kuunguruma. Muungurumo wake huwa na malengo ya kutangaza uwepo wake ktk himaya yake. Hufanya hivi ili kuwaarifu madume wengine wanaotangatanga kuwa yupo na wakae mbali na eneo hilo. Majike huwa na mlio tofauti na madume ambao lengo lake ni kuwaamrisha watoto alio nao

Siku ambayo hewa ni kavu (haina unyevunyevu) ngurumo za sharubu huweza kusikika umbali wa hadi kilometa 5. Kwa siku ambayo hali ya hewa ni ya unyevunyevu, sauti yake inaweza kusikika umbali wa kilometa 10.

No comments:

Post a Comment