Thursday, June 16, 2011

'Mateja' wa geti la Lodware - Ngorongoro crater

Eneo ambalo geti la Lodware ni eneo ambalo lina Nyani wengi. Kwa kipindi kirefu Nyani hawa wamejijengea tabia ya kukwapua vitu mbalimbali ambavyo vinaachwa wazi kwenye magari ya wageni au wakati mwingine kuwapora wageni vitu toka mikononi mwao. Kutokana na ka-tabia haka, mimi hupenda kuwaita Nyani hawa Mateja, nikiwafaninisha na jamaa wa mitaa ya huku mijini wanaokwapua simu na vitu vingine kwenye magari.
Mnapolikaribia geti la Lodware kuna tahadhari za msingi kabisa ambazo inabidi mzichukue kwa pamoja ili kuepusha tafrani ya namna yoyote na hawa mateja. Awali ya yote ni kuhakikisha ya kwamba vioo vya magari vinafungwa na pia roof ya gari inafungwa pia. Mateja hawa hutumia sehemu hizi kuingia ndani na kuchukua kile kitavutia kwenye mboni za macho yao.

Baada ya kufika geti ni vyema kuhakikisha kuwa milango ya magari haiachwi wazi kwani hiyo ni moja ya njia zao kuingia ndani. Pia, hakikisha mgeni haubebi kitu chenye muonekano unaofanana na lunch box. Nyani hawa wanajua kuwa wageni hubeba lunch box kwenye magari na lunch box hizi huwa na chakula kinachowafaa. hicho ndio kitu cha kwanza huwa wanaanza kukiandama kwenye magari. Wanapoona mtu (akiwa nje ya gari) kabeba lunch box au kitu kinachofanan na lunch box, basi mateja hawa hawatasita kumuandama. Mbaya zaidi ni pale mlengwa wao anapokuwa ni mdada au binti. Huwa wanawasumbua sana akina dada (bila kujali rangi au utaifa) kama inavyoonekana katika picha ya kwanza. Pembezoni mwa eneo la kuegeshea magari, kuna kichaka ambacho mateja hawa huenda kujichimbia na kufaidi kile wanachokwapua eneo la parking.

Hapo kama roof ya hilo gari ingekuwa wazi, huyu teja asingejali kama ndani kuna watu au la, angezama ndani ya hilo gari na kuanza kuchukua kile kinanchomvutia na kuondoka nacho kama anamudu kukibeba. Yapo matukio ya mateja hawa kubeba mifuko ya Camera za wageni na kisha kuzibwaga kwenye kichaka baada ya kubaini kuwa hazina dili kwao.

Huyo alikuwa kajificha kwenye kichaka akifanyia timing mlango wa gari ulioachwa wazi. Alikuwa anasubiri abiria ashuke au ajisahau asogee karibu na kulianzisha.

Dereva aliwahi kufunga kioo hivyo teja hili likaamua kuachana na jaribio lake la kuvamia gari hilo

akila vitu vilivyodondoshwa toka kwenye gari liliogeshwa hapo awali.

Kichaka chao cha kulia-timing na kupanga mashambulizi yao.
Mambo haya yanaweza kuonekana kama ni kero kwa wageni lakini ukweli ni kwamba sisi binadamu ndio tumeingia kwenye maeneo yao na kuingiza utamaduni ambao umepelekea mabadiliko ya tabia za hawa Nyani. Nyani hawa wameachana na utaratibu wao wa maisha ya kawaida wa kutafuta chakula maporini na badala yake wameamua kuweka kambi hapa kwenye geti la Lodware na kusubiri fursa ya kupora au kukwapua lunch box za wageni wanaopita eneo hili. Endapo mgeni atafuata ushauri anaopewa na guide wake basi anakuwa na fursa ya kupita salama. Endapo kipengele kimoja kisipofuatwa, basi utajikuta upo nao uso kwa uso. Ahsante ya picha kwa Mdau GBM aliyekuwa matembezini Ngorongoro crater hivi karibuni.

2 comments:

  1. thanks nilijua utaonyesha na njinsi wanavyokwapua vitu.!!!!

    ReplyDelete
  2. mbwembwe tu hana lolote! huna kazi ??

    ReplyDelete