Monday, May 16, 2011

TANAPA yakaribisha wawekezaji...

Tenda ya kukaribisha makampuni yanayojishughulisha na huduma za Balloon Safaris, kuja kufungua shughuli zao ktk hifadhi ya Mikumi na Ruaha. Uwepo wa Balloon Safaris ndani ya mikumi utatoa fursa kwa wageni wa ukanda wa kusini nao kuwa na sehemu ya kufanya Balloon safaris wanapokuwa nchini. Kwa sasa ni Serengeti na Tarangire ndio kuna huduma za Balloon safari.

Zabuni nyingine iliyotangazwa leo na TANAPA ni ya ujenzi wa mahoteli na parmanent tented camps ktk hifadhi zifuatazo - Kitulo, Mkomazi, Mikumi na Saadani. Kwa mujibu wa tangazo ambalo TembeaTz imekutana nalo ktk gazeti la Daily news (TZ) la leo, TANAPA inakaribisha makampuni yenye uwezo kutuma maombi yao kabla ya Tarehe 18 Agosti 2011.

Pata nakala yako ya Gazeti la leo la Daily News upate kujua zaidi

No comments:

Post a Comment