Monday, May 16, 2011

Kwihala Camp - Ruaha NP

Ni Moja ya campsites zinazomilikiwa na AdventureCamps Tanzania. Tented camp hii ipo ndani ya Hifadhi ya taifa ya Ruaha. Malazi hapa ni ndani ya mahema.

Unapokaa katika tented camps, unakuwa upo karibu mno na wenyeji wako. Hapa masikio huyu alipita kuwasabahi wageni wake akiwa katika pitapita zake ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Usiku ni mwendo wa kandili. Ina raha yake....


Hali ya hewa inaporuhusu, wageni wachache hupata fursa ya kula chakula cha usiku nje ya hema huku wakimulikwa na kandili sambamba na mwezi na nyota.

3 comments:

 1. Ebwana pako romantiki sana hapo.... ila tembo nao wakija kula msosi inakuwaje....

  ReplyDelete
 2. SV,
  Kwihala camp imetulia...
  Masikio kama hujamchokoza hana madhara, cha msingi ni kufuata do's-and-dont's unazoambiwa na wazoefu wa wanyama.

  ReplyDelete
 3. Picha ya usiku imetulia. ina maana hii campsite haina fence ili kuzuia wanyama wakali wasisogee karibu? huyo tembo yupo karibu sana

  ReplyDelete