Saturday, May 7, 2011

Gibbs Farm, Beho Beho na Nomads Mobile Camps zashinda ktk Safari Awards 2011

Jana jioni huko Durban, SA kulikuwa na shughuli ya kuwataja na kuwapa tuzo washindi walioingia ktk mchakato wa Safari Awards 2011. Tuzo hizi ziligawanya ktk vipengele 21. Hoteli mbili zilizopo Tanzania pamoja na kampuni moja nayo toka Tanzania zimeibuka na ushindi katika vipengele vitatu tofauti.

Gibbs Farm iliyopo huko Ngorongoro imeibuka mshindi ktk kipengele cha Best Safari Hotel in Africa. Ktk kipengele hiki Gibbs Farm ilikuwa ikichuana na Plantation Lodge (Ngorongoro Tanzania), Victoria Falls Safari Lodge na Emin Pasha. Ktk mbio hizi, Gibbs imeibuka mshindi huku Plantation Lodge ambayo nayo ni toka Tanzania imechukua nafasi ya pili.

Katika kipengele cha Best Safari Property in Eastern Africa, Beho Beho (Selous GR) imejinyakulia ushindi huku ikifuatiwa na Singita Sabora Camp (Grumeti Reserve, Tanzania). Katika mpambano huu, Beho beho ilikuwa ikichuana vikali na Hotel 3 zinazomilikiwa na kampuni ya Singita inayoendesha shughuli ktk pori tengwa la Grumeti. Hoteli hizo ni Singita Faru Faru, Singita Sasakwa na Singita Sabora Camp ambayo imechukua nafasi ya pili.

Nomad Tanzania Mobile Safaris
ya hapa Tanzania imeibuka mshindi kwenye kipengele cha Best Mobile Safari Operator in Africa. Kampuni ya Nomad inayoendesha campsite kadhaa zilizopo hapa Tanzania imeibuka mshindi dhidi ya kampuni nyingine tano ikiwemo Andbeyond Serengeti under Canvas nayo toka Tanzania. Kampuni ya Nomad Tanzania inaendesha campsites zifuatazo; Sand Rivers Selous, Kiba Point, Greystoke Mahale, Chada Katavi, Lamai Serengeti, Serengeti Safari Camp, Nduara Loliondo and Wilderness Mobile Camp.

Ukiachia mbali kampuni hizo kunyakua ushindi katika vipengele tajwa hapo awali, kampuni na hoteli nyingine za kitalii toka Tanzania zimeweza kuonyesha ushindani katika vipengele vingine na kutoa upinzani mkali kwa washindani wengine.
- Best Beach Safari Property in Africa - Fundu Lagoon, nafasi ya pili
- Best Safari Property in Africa - Beho Beho, nafasi ya tatu
- Best New Safari camp in Africa - The Retreat Selous, nafasi ya tatu.
- Best Safari Spa in Africa - Singita Faru Faru, nafasi ya tatu
- Best Air Charter in Africa - Coastal Aviation, nafasi ya tatu.

Kufungwa kwa pazia la awards za 2011 kunaashiria kufunguliwa kwa kurasa mpya kuelekea awards za 2012. Kwa walioshinda kazi itakuwa ni kuhakikisha wanaendelea kudumu na kudhihirishia uma kwamba waliowapa ushindi hawakufanya makosa. kwa wale walioukosakosa ni dhahiri ya kwamba wameonyesha upinzani na wananafasi ya kujipanga upya kwa mtanange ujao ili kuweza kuwapiku walioshindwa. Kwa zile Kampuni na hoteli zilizopo Tanzania ambazo hazikuingia kabisa kwenye mtanange wa mwaka huu kwa sababu zozote basi zianze kutathmini na kujipanga upya kwa 2012. Hoteli au kampuni inapotunukiwa zawadi ni neema kwa kampuni kwani inaashiria ubora ktk utendaji wake ktk kutoa huduma kwa wateja wake.

1 comment:

  1. Hongera sana kwa washindi wa mwaka huu wa Safari Awards 2011. Ni imani yangu kwao kuwa safari Award 2012 ushindi utakuwa kwao tena.

    Ila na wengine wajitokeze katika shindano hilo ambalo linatuletea sifa katika nchi yetu.'good will' itawasaidia katika kuwahudumia wateja wao.au mteja ni mfalume.

    ReplyDelete