Monday, April 11, 2011

Hawa ni makapela - Ngorongoro

Hawa sharubu wawili walikuwa ni makapera, ikiwa na maana ni masharubu dume ambao hawana teritory na hawamiliki majike.

Kikubwa kinachokuwa kwa makapera ni kutafuta dume mwenye majike, wapambane nae na baada ya kufanikiwa kumpiga (kumpindua) kuchukua umiliki wa majike wake. Wakikuta majike wana watoto wadogo, basi washindi hao huwauwa watoto hao ili kuwarudisha mama zao ktk hali ya kuwa tayari kupandwa - joto.


Walikuwa wamekula pozi pembezoni mwa barabara iliyopo 'shimoni' Ngorongoro crater kama ambavyo mdau Aenea wa Tanzania Giraffe Safaris alivyowakuta.

No comments:

Post a Comment