Monday, March 7, 2011

Warsha ya kuboresha utalii hapa Tanzania

Dr. Nzuki Mkurugenzi wa TTB akihutubia ktk mkutano uliowakutanisha wadau kadhaa wa Utalii kujadili namna ya kuboresha utalii hapa nchini na jinsi ya kuja na kauli mbiu ya kuinadi nchi yetu kama kivutio kwa watalii huko nchi za nje. Mkutano huu ulifanyika hivi karibuni ktk hoteli ya Double tree by Hilton, DSM.

Mgeni rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ezekiel Maige akizungumza ktk ufunguzi wa kikao cha kujadili namna ya kuboresha utalii hapa nchini kikao ambacho kilichofanyika jijini dar hivi karibuni. Moja ya mambo ambayo waziri alisisitiza ktk hotuba yake ya ufunguzi ni matumizi ya teknohama ktk kunadi vivutio vilivyopo hapa nchini.

Sehemu ya wadau walioshiriki mkutano huu wakifuatilia hotuba ya Mheshimiwa Waziri alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo.


Mheshimiwa waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige akifafanua jambo wakati alipohojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani).

1 comment:

  1. Nimegundua kuwa hata sisi wanablogu tuna nafasi kubwa ya kuitangaza nchi. Hii blogu ya Tembea Tanzania ni mfano hai. Inavutia.

    Nami najikongoja katika harakati hii. Kwenye blogu yangu ya ki-Ingereza, hii hapa, nimeandika taarifa kadhaa kuhusu sehemu kama Longido, Lushoto, Litembo, na Mbamba Bay, na nimeona kuwa taarifa hizo zinatembelewa na watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

    Nimewahi hata kupata barua pepe za watu wakiulizia zaidi kuhusu maeneo hayo, na kuna waJerumani fulani waliniulizia utaratibu wa kufika Mbamba Bay na mahali pa kukaa. Na kweli, hatimaye walisafiri na kuja nchini.

    Hii imenipa changamoto ya kuandika zaidi, sio tu makala nyingi zaidi, bali makala bora zaidi.

    ReplyDelete